Psalms 72:6-11

6 aAtakuwa kama mvua inyeshayo juu ya shamba lililofyekwa,
kama manyunyu yanyeshayo ardhi.
7 bKatika siku zake wenye haki watastawi;
mafanikio yatakuwepo mpaka mwezi utakapokoma.

8 cAtatawala kutoka bahari hadi bahari
na kutoka Mto
Yaani Mto Frati.
mpaka miisho ya dunia.
9Makabila ya jangwani watamsujudia,
na adui zake wataramba mavumbi.
10 eWafalme wa Tarshishi na wa pwani za mbali
watamletea kodi;
wafalme wa Sheba na Seba
watampa zawadi.
11 fWafalme wote watamsujudia
na mataifa yote yatamtumikia.
Copyright information for SwhNEN